Tuesday , 19 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Sababu ongezeko vifo ajali ya Lori Morogoro yaelezwa
Afya

Sababu ongezeko vifo ajali ya Lori Morogoro yaelezwa

Spread the love

HATUA ya majeruhi wengi wa ajali ya Lori la mafuta lililowaka moto Morogoro, walifikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimibi (MNH) kuendelea kupoteza maisha, ni kutokana na kuungua kwa asilimia 80 hadi 90. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Mpaka sasa majeruhi 32 kati ya 47 walifikishwa MNH, wamefariki dunia ambapo waliobaki 15 wote wako kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).

Ufafanuzi huo umetolewa leo tarehe 21 Agosti 2019 na Dk. Laurian Rwanyuma, daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali hiyo, na kwamba majeruhi wengi waliungua sehemu za ndani ikiwemo mfumo wa hewa na figo.

“Kuungua kwa ndani kumesababisha kupumua kwao kuwa kwa shida,.. kutokana na ngozi zao kuungua kwa asilimia kubwa, hali hiyo imesababisha mwili kukosa kinga na kupoteza maji mengi,” amesema Dk. Rwanyuma na kuongeza;

“Kwa kawaida wagonjwa walioungua kiasi hicho, wana uwezekano mdogo wa kupona hata kama hospitali ina uwezo mkubwa wa vifaa na dawa.”

Dk. Rwanyuma amewaeleza wanahabari kwamba, madaktari wanaendelea kufanya juhudi zao kuhakikisha majeruhi waliobaki wanapata afueni na kupona.

Mpaka sasa, tayari watu 100 katika ajali hiyo ilitokea tarehe 10 Agosti 2019, Morogoro wamefariki.

Related Articles

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

AfyaBiashara

Meridianbet yatoa msaada zahanati ya Mwenge

Spread the love MABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet wamefanikiwa kufika eneo...

AfyaTangulizi

Serikali yafafanua kuondolewa dawa 178 kitita cha NHIF

Spread the loveSERIKALI imesema imeondoa dawa 178 katika kitita cha Mfuko wa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Matende, mabusha tishio Kinondoni, wananchi waitwa kupata kinga tiba

Spread the loveMAGONJWA yasiyopewa kipaumbele ya Mabusha na Matende, bado yanaendelea kusumbua...

error: Content is protected !!