Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rungwe: Nikiwa rais, nitauza ndege za Magufuli
Habari za Siasa

Rungwe: Nikiwa rais, nitauza ndege za Magufuli

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
Spread the love

HASHIMU Rungwe, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chaumma amesema, iwapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, atauza ndege zilizonunuliwa hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mgombea huyo ambaye pia ni Mwentekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini.

“Kazi ya awali nitakayoifanya endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, nitauza ndege zilizonunuliwa hivi karibuni,” amesema.

Katika miaka mitano ya utawala wa Rais John Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amenunua jumla ya ndege zaidi ya saba.

            Soma zaidi:-

Miongoni mwa ndege hizo ipo Boeing 787-8  Dreamliner, Airbus A220-300 na Bombardier.

 

Sambamba na hilo, Rungwe akipata ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi amesema, atauza magari ya kifahari yanayotumiwa na serikali hususan yale ya wakuu wa wilaya na mikoa.

Mwanasiasa huyo pia amewaeleza Watanzania, kwamba yuko tayari kuwatumikia wananchi bila mshahara.

Rungwe ametoa kauli hiyo tarehe 2 Septemba 2020, wakati anahojiwa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, kuhusu biashara zake na harakati za kisiasa.

Katika mahojiano hayo, Rungwe aliulizwa kwa nini ameamua kugombea Urais badala ya kujikita katika biashara zake za uuzaji wa magari yaliyotumika, ambapo alijibu ameamua kugombea ili awatumikie Watanzania.

Rungwe ameeleza, hata kama watu wakisema hakuna mshahara yeye atakubali kuwa Rais wa Tanzania kwakuwa anahaja ya kuwatumikia Watanzania na Taifa lake.

“Watu wana vitu vingi wana biashara kubwa. Magari yana nini? Mimi nauza magari ndio biashara yangu we umeamua kuuza biashara ya simenti uza, watu wanaosena namna hiyo tuwaachie wazungumze, mimi nataka kutumikia nchi hata kama wakisema hakuna mshahara mimi nitatekeleza, nataka  kuwatumikia ,” amesema Rungwe.

1 Comment

  • Namkubali sana huyu mheshimiwa,
    Hana ugomvi na mtu
    Hamtukani mtu
    Yeye anatangaza sera ambazo hazitekelezeki,
    Ni mtu mwema sana kwa Rais wetu,
    Natamani kumsikiliza sera zake zinafurahisha,
    Hata kama umenuna uachekaaaa,
    Big up Hahim Rungwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!