Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rungwe kuzindua kampeni J’mosi Dar, aahidi ubwabwa
Habari za Siasa

Rungwe kuzindua kampeni J’mosi Dar, aahidi ubwabwa

Spread the love

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama cha Chaumma, Hashimu Rungwe, ametangaza kuzindua kampeni zake za urais wa chama hicho Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 Manzese jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chaumma amesema hayo leo Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online lililotaka kujua uzinduzi wa kampeni zake.

“Chaumma itaongea na wananchi 5 Septemba 2020 katika Uwanja wa Manzese Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Wananchi waje wasikilize, tunachowaambia. Wakija pale watapata kila kitu na watauliza maswali na tutawajibu,” amesema Rungwe

“Wako watu wenye hamu ya ubwabwa waje tutajua tunawapatiaje,” amesema

Rungwe ameahidi endapo akiingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, atarejesha mfumo wa zamani wa kugawa chakula kwa wanafunzi shuleni.

Amesema, Serikali atakakayoiunda itahakikisha inagawa wali (ubwabwa) kwa wanafunzi shuleni ili kuwawezesha kusoma na kuwawezesha kufaulu vyema masomo yao.

Rungwe amesema, hakuna mtu asiyependa ubwabwa na Serikali yake itahakikisha hilo linafanyiwa kazi kwani mtu akishiba anaweza kufanya kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!