Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rugemarila ataja wezi wa fedha za Escrow 
Habari za Siasa

Rugemarila ataja wezi wa fedha za Escrow 

James Rugemarila na Harbinde Seth (kulia)
Spread the love

MFANYABIASHARA James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja, Anaripoti Mwandishi wetu.. (endelea).

Amewataja watu hao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

“Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea TAKUKURU washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” – James Rugemarila

Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Tofauti na hayo Rugemarila pia ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini India kwa sababu anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi akiiaambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.

Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19, 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!