Rufaa ya Zombe kusikilizwa kesho

MAHAKAMA ya Rufani kesho inatarajia kusikiliza rufaa dhidi ya Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam (RCO) wa zamani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane, anaandika Faki Sosi.

Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) alikata rufaa hiyo namba 358 ya mwaka 2013, akipinga Zombe na wenzake kuachiwa huru na Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa ikiwakabili.

Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa leo Mahakama ya Rufani na jopo la Mmjaji watatu ambano ni Bernard Luanda, kiongozi wa jopo, na wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.

Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Koplo FestusGwabisabi.

Katika rufaa yake, DPP anapinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyowaachia huru wajibu rufaa hao katika kesi ya msingi ya mauaji, kwa madai kuwa Jaji alikosea kuwaachia huru kwani kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wote.

Awali Zombe na wenzake walikuwa wakidaiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge Morogoro na dereva mmoja wa teksi.

Wafanyabiashara hao Sabinus Chigumbi, (Jongo) na ndugu yake Ephrahim Chigumbi. Mwingine ni Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, ambaye alikuwa dereva teksi mkazi wa Manzese Dar es Salaam.

Watu hao waliauawa Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam, na ilidaiwa kuwa walikamatwa na washtakiwa hao wakiwa ha, eneo la Sinza.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyoteolewa na Jaji Salum Massati Agosti 17, 2009iliwaachia huru washtakiwa wote baada ya kuwaona kuw ahawana hatia kwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili na kwamba upande wa mashta ulishindwa kuthibitisha makosa hayo kwa washtakiwa bila kuacha mashaka.

DPP hakuridhika na hukumu hiyo na mwaka huohuo (Oktoba 6, 2009), alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akipinga hukumu hiyo ya Mahakama Kuu.

Alikuwa akidai kuwa Jaji Massati alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao, na kwamba kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa kimazingira wa kutosha kuwatia hatiani washtakiwa wote.

Rufaa hiyo hata hivyo ilitupiliwa ambali na Mahakama Mei 8, 2013 kutokana na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa hiyo, lakini baadaye DPP alipeleka maombi Mahakama Kuu aruhusiwe kukata tena rufaa hiyo nje ya muda, ambapo Mahamaka Kuu ilikubalia maombi yake.

MAHAKAMA ya Rufani kesho inatarajia kusikiliza rufaa dhidi ya Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam (RCO) wa zamani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane, anaandika Faki Sosi. Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) alikata rufaa hiyo namba 358 ya mwaka 2013, akipinga Zombe na wenzake kuachiwa huru na Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa ikiwakabili. Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa leo Mahakama ya Rufani na jopo la Mmjaji watatu ambano ni Bernard Luanda, kiongozi wa jopo, na wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage. Mbali na Zombe, wajibu rufaa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube