Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)- Taifa na Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini wamepelekwa mahakamani hapo leo tarehe 18 Februari 2019 kwa ajili ya kusililiza uamuzi ya rufaa yao.
Katika Barabara ya kwenda Kivukoni kuanzia kona ya Mahakama ya Rufaa hadi kona ya Mahakama Kuu, Jeshi la Polisi limeweka polisi wake huku wakitembea huku na kule wakiwa na mitutu jambo mbalo si kawaida.
Mbowe na Mtiko walifutiwa dhama yao tarehe 23 Novemba mwaka jana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kueleza kuwa, walikwenda kinyume na masharti ya dhamana kwenye kesi ya uchochezi inayowakibili.
Leo Februari 18 Mahakama hiyo itaamua aidha kubatilisha katazo la dhamana ya Mbowe na Matiko au kuendelea kusota mahabusu ambapo katika kesi ya msingi, washtakiwa ni Mbowe na Matiko.
Wengine ni Mbunge wa Peter Msigwa, Iringa mjini; John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji.
Pia wamo Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.
Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.
MwanaHALISI Online Ipo Mahakamani kukujuza kitachojirili kwenye uamuzi huo.
Leave a comment