Thursday , 28 March 2024
Habari za SiasaTangulizi

RITA mgomvi mpya CUF

Maalim Seif na Lipumba
Spread the love

CUF imetangaza rasmi leo kwamba Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuwa ni “mgomvi” mwingine katika mgogoro wa uongozi unaokikabili chama hicho kwa mwaka mzima sasa, anaandika Jabir Idrissa.

RITA, moja ya taasisi nyeti za dola, imeongezwa katika orodha baada ya kuthibitika imetumika kumsaidia Profesa Ibrahim Lipumba kusajili Bodi ya Wadhamini kwa lengo la kukivuruga chama.

“Ofisi ya RITA imejiunga na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi kukivuruga chama na kufuta matumaini ya Wazanzibari,” alisema Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF.

Ni katika nukta hiyohiyo, Maalim Seif amesema RITA imeingia katika mpango mchafu wa kuhakilisha haki ya Wazanzibari ya ushindi wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa 25 Oktoba 2015.

CUF inashikilia kuwa mshindi wa uchaguzi huo lakini umeporwa kwa mbinu za CCM kumtumia Jecha Salim Jecha, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Maalim Seif ametoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Peacock, Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.

Kuhusu haki hiyo, ametangaza kuwa ana matumaini makubwa kuwa itapatikana haipiti miezi mitatu kwa kuwa uchafu uliofanywa na RITA umeongeza nguvu ya madai ya Wazanzibari.

Huku akitaja vielelezo mbalimbali, vya mawasiliano kati yake na RITA na kati ya RITA na Msajili wa Vyama vya Siasa, Maalim Seif amesema Wakala wa Usajili amethubutu kughushi nyaraka ili tu kutii maelekezo ya Msajili Mutungi.

Nyaraka ambazo Maalim Seif amezieleza leo zinahusu hatua mbalimbali za kuhakikisha mpango mchafu wa serikali ya CCM kuhujumu chama hicho unaomhusisha pia Prof. Lipumba unafanikiwa.

RITA imeingizwa katika orodha ya wagomvi wa CUF kwa hatua yake ya kuidhinisha “bodi feki” ya wadhamini kupitia taarifa yake ya Juni 12 mwaka huu.

Kwenye taarifa hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson amemuarifu anayemtambua kama Kaimu km CUF, Magdalena Sakaya kuwa ombi lake la kusajili wa Bodi ya Wadhamini limekubaliwa.

Hudson ameeleza katika taarifa hiyo kuwa ameridhia ombi la Sakaya kwa kuwa hatua walizochukua ni sahihi na yeye ameziweka katika kumbukumbu za RITA.

Mwishoni mwa wiki, Hudson aliwaambia wahariri waliokutana Morogoro kwamba aliidhinisha Bodi iliyoombwa na Sakaya kwa “maelekezo ya Msajili wa Vyama ambaye ndiye maimamizi wa vyama vya siasa nchini.”
Maalim Seif amesema leo kuwa Prof.

Lipumba si mwanachama wa CUF na kwa hivyo hana nafasi ya kushughulikia masuala yoyote yanayokihusu chama hicho.

Kwa muda wote wa CUF kugubikwa na mgogoro baada ya Prof. Lipumba kuamua kutengua uamuzi wa hiyari yake wa kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti Agosti mwaka juzi, CUF imekuwa ikimtaja moja kwa moja Msajili Vyama kuwa ndiye chimbuko la mgogoro.

Lakini sasa RITA kwa hatua ya kukubali kutumika, amesema Maalim Seif, imejiingiza ndani na kwa sababu hiyo italazimika kujieleza mbele ya Mahakama.

Maalim Seif amesema chama kitamshitaki CEO wa RIta na hapo mawakili watataka kesi hiyo isikilizwe huku zile nyingine zikisotishwa kwanza.

 

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!