Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya CAG: Zitto amvuruga Spika Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

Ripoti ya CAG: Zitto amvuruga Spika Ndugai

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, anamtuhumu Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe, kujitafutia umaarufu wa kisiasa, kupitia Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni mjini Dodoma labla ya kuahirisha bunge mpaka mchana wa leo tarehe 25 Aprili 2019, Ndugai amedai kuwa, Zitto anatumia taarifa zilizomo kwenye ripoti ya CAG, kuchambua ripoti hiyo ili aonekane ‘shujaa’.

Spika Ndugai amesema, anachokifanya Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, kuaminisha wananchi sio sahihi kwa madai kuwa, si kila kilichomo kina kweli.

Zitto kwenye majukwaa mbalimbali amekuwa akifanya uchambuzi wa ripoti hiyo ya Mwaka wa Fedha 2017/18 katika majukwaa ambapo Spika Ndugai amesema, “aache kuuaminisha umma kuwa, kila kilichoandikwa kwenye Ripoti ya CAG ni kweli.”

Maeneo ambayo Zitto amekuwa akiyachambua kwenye majukwaa hayo ni pamoja na;-Shilingi 4.8 Trilioni Zimetumika Bila Kupita Kwenye Mfuko Mkuu, Serikali Imeanza Kushindwa Kulipa Madeni (Defaulting), Mikopo ya Ndani Yashindwa Kulipa Madeni Kikamilifu na Kushuka kwa Thamani ya Shilingi Kunakuza Zaidi Deni la Taifa.

Spika Ndugai amesema kuwa, wapo Watanzania wanaoamini kwamba, kila kilichoandikwa kwenye ripoti ya CAG yana ukweli kwa asilimia mia moja “jambo hili sio kweli.”

“…watu wanawaaminisha Watanzania kuwa kila kilichoandika kwenye na CAG mle ni ukweli kwa asilimia mia moja. Yapo mambo mle ambayo si kweli hata kidogo, tena mengi tu,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai amesema kuwa, Zitto amekuwa akibeba taarifa zilizoandikwa kwenye kitabu cha CAG kama zilivyo ili kuwaaminisha wananchi kwamba, ana uwezo mkubwa wa kuchambua.

Amefafanua kuwa, hata halmashauri yake inayoongozwa na ACT-Wazalendo mkoani Kigoma, imetajwa kuwa na hati chafu na kwamba, kila mtu aliyetajwa ataitwa kujieleza.

Akizungumzia utaratibu Spika Ndugai amesema, kwa utaratibu wa kawaida, taarifa ya CAG baada ya kuwekwa mezani, hupelekwa katika Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LLAC).

“Kwenye kamati kule, watachambua hoja baada ya hoja,” amesema Spika Ndugai na kwamba, kila anayetajwa atalazimika kuitwa na kutoa maelezo.

Hata hivyo, Spika Ndugai ameeleza kuwa, Zitto kufanya uchambuzi huo si kosa kwa kuwa, hajavunja kanuni yoyote.

“Mimi nadhani sio sahihi kwa Spika Ndugai kumzungumzia Zitto hasa kwa kile anachokifanya, maana Zitto anazungumzia nje ya Bunge.“Malalamiko hayo yangetolewa na serikali-Waziri Mkuu ama mawaziri – hapo sawa kwa kuwa, Zitto anazungumzia serikali na sio Bunge.

“Ninachoona hapa ni kuwa, Bunge linaunganishwa na serikali, jambo hili ni hatari sana,” amezungumza mbunge wa CCM aliyeomba kutotajwa jina lake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!