UCHUNGUZI wa awali wa afya ya George Floyd umeonesha kwamba, alikuwa na maambukizi ya virusi vinavyosababisha homa kali ya mapafu corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).
Ripoti iliyotolewa jana jioni Jumatano tarehe 3 Juni 2020 na Andrew Baker, Tabibu Mkuu wa Taifa imeeleza, Floyd alipimwa tarehe 3 Aprili 2020 na kubainika ameambukizwa corona.
Pia, ripoti hiyo imeeleza, mapafu ya Floyd yalikuwa na afya lakini kwenye moyo wake kulibainika kuwa na tatizo kidogo.
Na kwamba, mwili wake umekutwa na sumu kutokana na matumizi ya vinywaji ingawa inabainishwa, kuwa haiwezi kuunganishwa kwenye kifo chake.
Imeelezwa, sumu hiyo mwilini mwake inaweza kuchangia tatizo la upumuaji na mshutuko kutokana na tukio alilokutana nalo.
Pia, Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza amesema ‘maisha ya Waafrika ni muhimu’ na kwamba, hasira walizonazo Wamarekani ndizo walizonazo watu duniani kote.
“Bila shaka, maisha ya Waafrika ni muhmimu na ninaelewa hasira inavyotawala vifua sio kwa Wamarekani pekee, bali hapa kwetu na duniani kote kutokana na tukio la polisi wa Marekani kumuua Floyd.”
“Nakubaliana na maandamano yanayofanywa kupinga mauaji hayo, lakini nukta muhimu ni kuwa maandamano lazima yafanywe kwa kufuata sheria.”
Pia, Serikali ya Ujerumani imeeleza kujifunza kutokana na kile kinachoendelea Marekani. Msemaji wa serikali hiyo Steffen Seibert, amesema, Serikali hiyo imeshtushwa na mauaji hayo yaliyofanywa na maofisa wa serikali.
“Kifo cha George Floyd, kimeshtua hapa Ujerumani na sehemu yote ya dunia. Imeshtua sana Serikali serikkali yetu ya shirikisho, kile ni kifo kilichoweza kuzuilika,” amesema Seibert.
Leave a comment