January 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

RC Mghwira: Tutengeneze condom zetu

Anna Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro (RC), Anna Mghwira ameishauri Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), kuangalia uwezekano wa kuweka mikakati ya kutengeneza kondom wenyewe ili kuacha utegemezi wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Mghwira ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 24 Novemba 2020 wakati akizungumza katika mkutano ulioitishwa na TACAIDS na kuwakutanisha waandishi wa habari wa mkoani humo kuelekea siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani ambayo Kitaifa yatafanyika Kilimanjaro.

Aidha amesema, maadhimisho hayo yatafanyika viwanja vya shule ya msingi Mandela vilivyopo Mjini Moshi Desemba mosi.

“Tuweke mikakati mbalimbali ambayo tunaweza tukafanya na kuhakikisha tunategeneza condom zetu sisi wenyewe, ukiangalia madawa yote ya tiba yanatoka nje, condom zote zinatoka nje, sisi tunafanya nini ? tunabaki tuu kuwa wapokeaji wakati wataalam tunao?”

“Tunabaki tuu kuwa watu wa maneno na sio wa vitendo ,kama bidhaa hii inauzika vya kutosha ni lazima tuje na mkakati wa kutengeneza baadhi ya vifaa tiba na tusiwe watu wa kupokea tuu,” amesema Mghwira

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Leonard Maboko amesema idadi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini yanaendelea kupungua ambapo mwaka 2017 maambukizi mapya yalikuwa 72,000 ukilinganisha na mwaka 2019 ambapo yalikuwa 68,400.

“Takwimu zinaonyesha maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yanapungua nchini ambapo mwaka 2017 yalikuwa 72,000 ukilinganisha na mwaka huu ambapo maambukizi mapya ni 68,400 , idadi ya maambukizi inaendelea kupungua kutokana na watu wamejitambua,” amesema Maboko

“Hawa wote waliombukizwa virusi vya Ukimwi wakiendelea kupatiwa dawa (ARV’S) wanaishi maisha marefu ndio maana idadi ya wanaoishi inaendelea kuongezeka ,” a esema Maboko.

“Miaka ya nyuma takwimu zinaonyesha watu walikuwa wanaendelea kufa kwasababu ya virusi vya ukimwi ambapo mwaka 2001 walikufa watu 85,000 na mwaka 2019 walikufa watu 25,000 idadi ya vifo vitokanavyo na maambukizi ya Ukimwi yanaendelea kupungua kutokana watu kutumia (ARV’S),” amesema Maboko

“Kila mtu aliyeambukizwa virusi vya Ukimwi akatumia vizuri ARV’S uwezo wake wakumwambukiza mtu mwingine unapungua, hii ni hatua nzuri na inatia moyo,” amesema.

error: Content is protected !!