Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Mghwira awapa somo wanasiasa wanaotafuta kura
Habari za Siasa

RC Mghwira awapa somo wanasiasa wanaotafuta kura

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzanmia, Anna Mghwira amewataka wanasiasa kutumia majukwaa yao ya kisiasa kutoa matamko ya matumaini kwa wananchi ili kuisadia nchi isonge mbele zaidi badala ya kutumia majukwaa kutoa lugha za matusi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Anna amesema hayo hivi karibuni akiwa nyumbani kwake wakati akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM 2020 akisema, kipindi hiki kikitumiwa vizuri na wanasiasa kinasaidia kuwaweka wananchi pamoja lakini kikitumika vibaya kinaleta mfarakano na vurugu.

“Jukumu la wanasiasa kipindi hiki ni kuwaambia wananchi wataongeza thamani gani katika mambo yanayowagusa, maana vitu tayari vipo kinachotakiwa sasa ni kuboresha na kukarabati,” alisema Anna ambaye mwaka 2015 aligombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo.

Alisema dhamira ya serikali ya Mkoa ni kuhakikisha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara ili kuwezesha amani inakuwepo kabla na baada ya uchaguzi.

Anna alisema, hali ya usalama kwa sasa ni nzuri na hakuna vitisho vyovyote na kusisitiza kuwa wamejiandaa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na kwamba hadi sasa hakuna vitisho vyovyote vya uvunjifu wa amani.

“Matamanio ya wanasiasa ya jukwaani yatafsirike kwenye maeneo watakayokuwa wanayaongoza, watambue hawaji kuongoza watu wapya bali ni watu wale wale waliokuwepo,” alisema.

Kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mkoa huo kupitia uongozi wa serikali ya awamu ya tano alisema kiasi cha Sh.40.3 bilioni kimetumika kwa ajili ya kugharamia elimu bila ya malipo mkoani humo.

Aidha alisema, kiasi cha zaidi ya Sh.19 bilioni na sekondari zaidi ya Sh.43 bilioni kimetumika katika ukarabati wa miundombinu katika shule.

“Upande wa miundombinu ya barabara kiasi cha Sh.17 bilioni kimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa barabara, ujenzi wa hospitali mpya ya Rombo na Siha na Sh.12 bilioni kimetumika kukarabati pia jengo la mama na mtoto,” alisema

Mkuu huyo wa mkoa alisema, wanafuatilia viwanda ambavyo havijaendelezwa mkoani humo na kusisitiza mali za Watanzania zitarudi kwa watanzania.

Akielezea upande wa sekta ya maji alisema kiasi cha Sh.18 bilioni zimetumika katika kuhakikisha wananchi wanapata maji.

“Upande wa mifugo na kilimo tuna mpango wa kuwachimbia visima wafugaji ili mifugo yao ipate maji, ukiangalia wilaya ya Mwanga ndio inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafugaji hivyo maji ni muhimu kwao,” alisema.

Wakati huo huo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Jonathan Mabihya, alisema ushindi wa chama hicho kwa Mkoa huo mwaka huu ni zaidi ya asilimia 99 kutokana na wananchi kuielewa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ilivyofanga maajabu makubwa kwa kipindi kifupi tu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!