January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

RC Kunenge atangaza fursa za biashara Dar

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Aboubakar Kunenge amewataka wafanyabishara kuchangamkia fursa ya baishara katika Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Lius jijini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kituo hicho kitakachokuwa kikuhudumia mabasi ya mikoani na yanayokwenda nje ya mipata ya Tanzania, ujenzi wake umefikia asilimia 90.

RC Kunenge amesema hayo leo Jumatatu tarehe 9 Novemba 2020 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, majaribio ya kituo hicho itakuwa tarehe 25 Novemba 2020 na kutumika rasmi 30 Novemba.

Mkuu huyo wa mkoa, ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye kituo hicho ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hotel.

Kunenge amewataka wananchi wanaohitaji maeneo kutuma maombi kuanzia leo Jumatatu hadi tarehe 25 Novemba 2020.

Amesema, uwepo wa kituo hicho kitaendelea kufungua fursa za maendeleo kwa wakazi wa Ubungo hivyo amewataka kujiandaa kwa hilo.

error: Content is protected !!