Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Trump, mkewe waambukizwa corona 
Kimataifa

Rais Trump, mkewe waambukizwa corona 

Donald Trump, Rais wa Marekani
Spread the love

RAIS wa Marekani, Donald Trump na mkewe Melania Trump, sasa wapo karantini baada ya kukumbwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti BBC … (endelea).

Kabla ya Trump na mkewe kukutwa na corona, wasaidizi wake wawili walipimwa na kubainikwa kuambukizwa virusi hivyo.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Trump amethibitisha yeye na mkewe kukumbwa na virusi vya ugonjwa huo akisema ‘anajiweka karantini kwa siku 14.’

Pia Melania (50) kwenye ukurasa wake wa twitter ameandika.

Donald Trump na mkewe

”Kama ambavyo raia wengi wa Marekani wamefanya mwaka huu, Rais Trump na mimi tuko kwenye karantini nyumbani baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

“Tunaendelea vizuri na nimeahirisha shughuli zote zijazo. Tafadhali hakikisha uko salama na tutashinda changamoto hii pamoja.”

Hope Hicks (31) ambaye ni mshauri wa Trump, ndio msaidizi wa kwanza wa rais kukumbwa na virusi hivyo.

Wawili hao (Trump na Hicks) walisafiri pamoja wakati Trump alipokwenda kwenye mdahalo wa Televisheni alipokabiliana na mpinzani wake Joe Biden Jumanne wiki hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!