Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Rais, Spika na Jaji Mkuu hawatoshitakiwa Tanzania’
Habari Mchanganyiko

‘Rais, Spika na Jaji Mkuu hawatoshitakiwa Tanzania’

Spread the love

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamepinga muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali nchini namba 3 wa mwaka 2020. Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

THRDC na LHRC wametoa tamko la kupinga muswada huo leo Alhamisi tarehe 4 Juni 2020 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema katika mswada huo kuna marekebisho ya Sheria ya utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu ya 1994 (BRADEA).

Olengurumwa amesema, marekebisho ya kifungu Kifungu namba 4 cha BRADEA kinarekebishwa na kusomeka kwamba, maombi ya kufungua kesi Mahakama Kuu hayatakubaliwa endapo hayajaambatanishwa na kiapo cha mlalamikaji kuelezea jinsi alivyoathiriwa na uvunjifu wa haki na wajibu katika ibara ya 12 hadi 29 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

“Tumekuwa tukipeleka kesi ya kulalamika ukiukwaji wa haki za binadamu uliopo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 12 mpaka 29, sasa kwa mujibu wa mabadiliko ambayo yanakuja sasahivi ni lazima uwe na cheti cha kiapo cha kuonyesha kiasi gani wewe mwenyewe umeathirika na ukiukwaji huo,” amesema.

Amesema, Kifungu namba 7(4), ikiwa malalamiko ya uvunjifu wa haki unaelekezwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu wa Tanzania, malalamiko hayo yatafungliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali ikiwa na maana hakutakuwa na uwezekano wa kufungua kesi dhidi ya viongozi hao.

“Sasa hivi, tuna kesi nyingi tumefungua dhidi ya Spika na kuna kipindi Rais alifunguliwa kesi na akina Fatma Karume na Ado Shaibu hizo zote zitaondolewa maana yake Tanzania hatutaweza kumshtaki mtu kama yeye kwa kukiuka Katiba,” amesema.

Aidha, Olengurumwa amesema sheria nyingine ambayo inaelekea kufanyiwa mabadiliko ni sheria ya uongozi wa Mahakama namba nne ya 2011.

Amesema, kifungu namba 64 (a) cha sheria hiyo kimerekebishwa na kuandikwa kuwa mfanyakazi yoyote wa mahakama hatoshtakiwa kwa jambo lolote atakalolifanya au kutolifanya kwa nia njema atakapikuwa anatekeleza majukumu yake.

“Hii inaweka kinga kwa mtu yoyote alioko mahakamani hata kama si Jaji au Hakimu na madhumuni ya marekebisho hayo ni kuipa mahakama nguvu ya kukataa maombi ambayo hayajakidhi matakwa ya ibara wao ndio wanadai hivyo.”

“Madhumuni ya marekebisho haya yanakwenda kuondoa nguvu za mtu mmoja mmoja au taasisi kama zakwetu kufungua kesi kwa sababu ya kulinda haki zozote zinazokiukwa Tanzania na hii ni kinyume na ibara ya 26 ya Katiba ya Tanzania ambayo imemruhusu mtu yoyote kwenda mahakamani kudai haki,” amesema.

Kwa upande wake, Anna Henga, Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, amesema mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya utekelezaji wa haki za msingi na wajibu yanapingana na ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa (wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga (wapili kulia).

“Baada ya Tanzania kujitoa kwenye mahakama ya Afrika sasa Azaki hatuwezi kwenda huko sasa hata kwenye mahakama za ndani hatutaweza kwasababu sheria hii inaweza kuzuia haki hiyo,” amesema.

Hata hivyo, Henga amesema marekebisho anayaona kama ni muendelezo wa kutaka kunyima haki kwasababu hata sababu za Tanzania kujitoa katika mahakama ya Afrika hazijajulikana hadi sasa.

“Ni kitu cha ajabu sana kwamba Afrika Mahakama ipo nyumbani kwako kama inakuletea heshima wewe ndo unayeitunza halafu unajitoa kwanini? hata hii, unaweza ukashangaa ni kwanini wazuiwe watu ambao wanataka kutetea haki za watu?  Ukitafsiri kikawaida maana yake haki itavunjwa zaidi,” amesema.

THRDC na LHRC wametoa wito kuwa mapendekezo hayo ya mabadiliko ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu yaondolewe kabisa Bungeni kwakuwa maandalizi ya mapendekezo hayo hayakuhusisha
kabisa wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa haki za binadamu tangu mwanzo.

Aidha, wamesisitiza kuwa kifungu cha mapendekezo ya sheria kinachotaka kutoa kinga kwa wafanyakazi wote wa Mahakama kutokushtakiwa kirekebishwe na kinga hiyo iendelee kuwepo kwa Majaji na Mahakimu pekee kwa mujibu wa Katiba.

Muswada huo unaopendekeza mabadiliko makubwa ya sheria mbalimbali ambayo THRDC na LHRC wanalaani wakieleza kuwa yanalenga kuondoa haki ya kufungua kesi za kikatiba kwa niaba ya wananchi, uliwasilishwa bungeni na umepangwa kujadiliwa kwenye mkutano wa 19 wa Bunge (Mkutano wa Bajeti) ambao ulianza tarehe 05 Mei na utamalizika
Juni 19 mwaka 2020.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!