Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Shein: Wazanzibar msijaribu uongozi
Habari za Siasa

Rais Shein: Wazanzibar msijaribu uongozi

Dk. Ali Mohamed Shein
Spread the love

ALI Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake, amewataka wananchi wa visiwa hivyo, kutofanya makosa kwa kumchagua Rais mwenye tamaa na asiyekuwa na uwezo wa kuongoza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Shein amesema hayo leo Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 wakati akimnadi Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uwanja wa Demokrasia- Kibandamaiti.

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utafanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hizo, Rais Shein amewataka wafuasi wa chama hicho na Wazanzibar kwa ujumla kutojaribu uongozi.

“Msije mkafanya makosa kujaribu uongozi kumpa mtu asiye na uwezo, mwenye tamaa yake binafsi, tumchague Dk. Hussein Mwinyi tutapata manufaa makubwa.”

“Pale ninapoachia mimi hapatamshinda yeye ataunganisha kwa kasi, atafanya yale anayoweza na ya kwenye ilani kwa asilimia mia,” amesema Dk. Shein.

Rais huyo wa Zanzibar anayemaliza muda wake, amempigia chapuo Dk. Mwinyi kwa wananchi akitaka achaguliwe kwa maelezo kwamba ana sifa zote za kuwa kiongozi.

“Nafahamu Mwinyi ana sifa zote za kuwa kiongozi wa CCM na Zanzibar, ana sifa za kuwa Rais wa Zanzibar bila mushkeri na mi nasema haya sababu hivi sasa ni rais, nafahamu kama akichaguliwa ataiongoza vizuri,” amesema Dk. Shein.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!