Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Robert Mugabe afariki dunia
Kimataifa

Rais Robert Mugabe afariki dunia

Marehemu Robert Mugabe enzi za uhai wake
Spread the love

ROBERT Mugabe, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zimbabwe, amefariki dunia. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya familia ya gwiji huyo wa siasa, ambaye alikuwa mpigania uhuru wa nchi hiyo zimeeleza,  kiongozi huyo amefariki dunia nchini Singapore baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais Mugabe alipigania uhuru wa  Zimbabwe ambayo ilipata uhuru tarehe 18 Aprili 1980.

Aliliongoza taifa hilo kwa takriban miongo mitatu, hadi alipoondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi Novemba 2017.

Aliyechukua nafasi yake ni aliyekuwa makamu wake wa rais, Emmerson Mnangagwa na baadaye wa rais, badadaye  alichaguliwa kuwa rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2019.

Fadzayi Mahere, Waziri wa Elimu wa Zimbabwe, ametoa taarifa ya kifo cha Mugabe kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika “Pumzika kwa amani Robert Mugabe.”

Robert Mugabe pia aliwahi kufungwa jela kwa zaidi ya muongo mmoja bila kufunguliwa kesi, ni baada ya kuikosoa Serikali ya Rhodesia mwaka 1964.

Naye Rais Mnangagwa ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter kuhusu kifo cha Mugabe na kusema kuwa, mchango wake hautasaulika.

“Mchango wake katika historia ya Taifa letu kamwe hautasaulika. Roho yake ipumzike kwa amani ya milele,”amesema.

Rais Mugabe alizaliwa Februari 21, mwaka 1924 katika nchi hiyo wakati huo ikiitwa Rhodesia na ameacha mke  ambaye ni Grace Mugabe na watoto wanne ambo ni Bona Mugabe, Chatunga Bellarmine Mugabe, Robert Peter Mugabe Jr., Michael Nhamodzenyika Mugabe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!