Pierre Nkurunziza, Rais mstaafu wa Burundi

Rais Nkurunziza afariki dunia

Spread the love

RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Taarifa zilizothibitishwa na Msemaji wa Serikali, Balozi Willy Nyamitwe, zimeeleza kuwa Rais Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo na serikali imetangaza siku saba za maombolezo.

Kupatikana kwa taarifa za kifo cha Rais Nkurunziza kinachodaiwa kusababishwa na “mshtuko wa moyo,” kumekuja takribani wiki mbili tangu kuthibitika kuwa mkewe, Denise Nkurunzinza, ameugua ugonjwa wa Corona.

Denise alikuwa amelazwa katika hospitali ya Aga khan jijini Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kusafirishwa kutoka Burundi, tarehe 1 Juni 2020.

Nkurunziza aliyezaliwa tarehe 18 Desemba 1963, aliingia madarakani mwaka 2005, kufuatia mkataba wa amani wa Arusha, nchini Tanzania.

Alichaguliwa tena kuwa rais katika uchaguzi wa uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu ofisini, mwaka 2015.

Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi

Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena nafasi hiyo, jambo ambalo lilisababisha maandamano na vifo vya watu kadhaa, ikiwamo kuzalisha wakimbizi.

Nkurunziza alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, alitangaza katika madaraka ya rais mara baada ya uchaguzi wa Mei mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Burundi, Nkurunziza alipewa hadhi ya kuwa ”Kiongozi Mkuu wa Burundi, mara atakapoondoka madarakani.

Bunge la nchi hiyo ndogo katika ukanda wa Afrika Mashariki, lilipigia kura muswada wa sheria wa kumpatia Nkurunziza cheo cha “Kiongozi Mkuu” na “Bingwa wa Uzalendo.”

Wabunge ambao wengi wao wanatoka chama chake cha CNDD-FDD, walipitisha azimio hilo ambalo baadaye lilipata baraka za Baraza la Mawaziri.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulifanyika katika jimbo la kisiasa la Gitega nchini Burundi.
Aidha, Bunge liliridhia pia kumlipa Bwana Nkurunziza, kitita cha faranga za Burundi 1 bilioni, mara atakapoondoka madarakani.

Burundi ilifanya uchaguzi wake mkuu, Mei mwaka huu, ambapo Jenerali mstaafu Evariste Ndayishimiye, alitangazwa kuwa mshindi.

Hata hivyo, aliyekuwa mgombea wa upinzani, Agathon Rwasa, amepinga ushindi wa Ndayishimiye kwa maelezo kuwa uchaguzi huo, ulitawaliwa na hila na udanganyifu.

Kufuatia madai hayo, Bwana Rwasa amefungua shauri mahakamani kupinga ushindi wa mpinzani wake, ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na “wizi wa kura” aliyodai umefanywa na wafusi wa Ndayishimiye.
Mapema mwaka huu, Nkurunziza aliitisha kura ya maoni na baadaye kuipigia chapuo iliyolenga kufanyika marekebisho katiba ya kubadilisha muhula wa rais kutoka miaka mitano hadi saba.

Hadi anafariki dunia, Rais Nkrunziza na serikali yake wamemekuwa wakishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu, mauwaji na ukatili dhidi ya binadamu.

RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, Inaripoti Mitandao ya Kimataifa...(endelea). Taarifa zilizothibitishwa na Msemaji wa Serikali, Balozi Willy Nyamitwe, zimeeleza kuwa Rais Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo na serikali imetangaza siku saba za maombolezo. Kupatikana kwa taarifa za kifo cha Rais Nkurunziza kinachodaiwa kusababishwa na "mshtuko wa moyo," kumekuja takribani wiki mbili tangu kuthibitika kuwa mkewe, Denise Nkurunzinza, ameugua ugonjwa wa Corona. Denise alikuwa amelazwa katika hospitali ya Aga khan jijini Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kusafirishwa kutoka Burundi, tarehe 1 Juni 2020. Nkurunziza aliyezaliwa tarehe 18 Desemba 1963, aliingia madarakani mwaka 2005,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!