Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Rais Mwinyi kutangza mawaziri kesho

Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi kesho Alhamisi tarehe 19 Novemba 2020, ataweka wazi sura ya baraza lake jipya la mawaziri. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Dk. Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, atakuwa anaunda baraza hilo la kwanza tangu alipoingia madarakani tarehe 2 Novemba 2020.

Rais Mwinyi aliingia madarakani akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Dk. Ali Homahed Shein aliyemaliza miaka kumi ya utawala wake kwa mujibu wa Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Hassan Hassan, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Habari, Ikulu imesema, Rais Mwinyi atatangaza baraza hilo, kesho Alhamisi saa 4:00 asubuhi

Taarifa hiyo ya uteuzi, imezidisha presha kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuona nani atateuliwa ili kuanza safari ya miaka mitano ya kuwatumikia Wazanzibar kwenye nafasi watakazoteuliwa.

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi kesho Alhamisi tarehe 19 Novemba 2020, ataweka wazi sura ya baraza lake jipya la mawaziri. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Dk. Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, atakuwa anaunda baraza hilo la kwanza tangu alipoingia madarakani tarehe 2 Novemba 2020. Rais Mwinyi aliingia madarakani akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Dk. Ali Homahed Shein aliyemaliza miaka kumi ya utawala wake kwa mujibu wa Katiba. Taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Hassan Hassan, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Habari, Ikulu imesema, Rais Mwinyi atatangaza baraza hilo, kesho Alhamisi saa 4:00 asubuhi Taarifa hiyo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!