Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi asamehe wafungwa 49
Habari za Siasa

Rais Mwinyi asamehe wafungwa 49

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Hussein Mwinyi, ametoa msamaha kwa wafungwa 49, waliokuwa wakitumikia magereza ya Unguja na Pemba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Msamaha huo unakwenda sambamba na shamra shamra za sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika leo Jumanne tarehe 12 Januari 2021.

Rais Mwinyi ametoa msamaha huo kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kinachompa mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa waliofungwa gerezani.

Kutokana na msamaha huo, Rais Mwinyi ameamuru kifungo kilichobaki cha wafungwa hao walionufaika na msamaha kuwa kipindi hicho chote kinafutwa na waachiwe huru kuanzia jana Jumatatu tarehe 11 Januari 2021.

Kati ya wafungwa hao 49; 46 walikuwa magereza ya Unguja na watatu Pemba.

Msamaha huo hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za Mapinduzi matukufu, huwahusisha wafungwa ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu au wenye makosa madogo ambao wamebakisha muda mfupi wa kutumikia adhabu zao, wanaoonesha nidhamu nzuri chuoni na kujutia makosa yao.

Wafungwa wenye makosa kama vile kuua kwa makusudi, wizi wa kutumia nguvu, wizi wa mali ya umma, makosa ya kudhalilisha wanawake na watoto, makosa ya dawa za kulevya na wenye makosa mengi ya zamani kwa kawaida huwa hawapewi msamaha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!