January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mwinyi amtumbua aliyemwapisha siku 37 zilizopita

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Spread the love

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ametengua uteuzi wa Katibu wake, Suleiman Ahmed Saleh. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 14 Desemba 2020 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Abdulhamid Mzee imesema, Saleh atapangiwa kazi nyingine.

Rais Mwinyi amechukua uamuzi huo zikiwa zimetimia siku 37 tangu alipomwapisha Saleh tarehe 7 Novemba 2020 kushika wadhifa huo.

Saleh aliteuliwa na Rais Mwinyi, tarehe 4 Novemba 2020 kushika wadhifa huo. Kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya pamoja ya Fedha.

Salehe amekuwa mteule wa kwanza wa Rais Mwinyi kuteuliwa na kutenguliwa tangu alipoingia madarakani tarehe 2 Novemba 2020 akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ali Mohamed Shein aliyemaliza muda wake wa uongozi kwa mujibu wa Katiba.

error: Content is protected !!