Yoweri Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda

Rais Museveni kumfuata Rais Magufuli kesho

Spread the love

YOWERI Museveni, Rais wa Uganda anatarajiwa kutua kwenye ardhi ya Tanzania kesho 13 Julai 2019, kwa ziara ya siku moja. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Taarifa ya Kurugenzi ya Ikulu iliyotolewa leo tarehe 12 Julai 2019 imeeleza kuwa, Rais Museveni anatarajiwa kuja Tanzania kumtembelea Rais Magufuli nyumbani kwake wilayani Chato, Mkoa wa Geita.

Rais Museveni na Rais Magufuli watakuwa na mazungumzo na baada ya siku moja, Rais Museveni atarudi Uganda.

Safari ya Rais Museveni imetanguliwa na ile ya Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya aliyekuja nchini siku chache zilizopita na kumtembelea Rais Magufuli nyumbani kwake Chato.

YOWERI Museveni, Rais wa Uganda anatarajiwa kutua kwenye ardhi ya Tanzania kesho 13 Julai 2019, kwa ziara ya siku moja. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Taarifa ya Kurugenzi ya Ikulu iliyotolewa leo tarehe 12 Julai 2019 imeeleza kuwa, Rais Museveni anatarajiwa kuja Tanzania kumtembelea Rais Magufuli nyumbani kwake wilayani Chato, Mkoa wa Geita. Rais Museveni na Rais Magufuli watakuwa na mazungumzo na baada ya siku moja, Rais Museveni atarudi Uganda. Safari ya Rais Museveni imetanguliwa na ile ya Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya aliyekuja nchini siku chache zilizopita na kumtembelea Rais Magufuli nyumbani kwake Chato.

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!