Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Mstaafu Mauritania akamatwa, ahojiwa kwa rushwa
Kimataifa

Rais Mstaafu Mauritania akamatwa, ahojiwa kwa rushwa

Mohamed Ould Abdel Aziz
Spread the love

MOHAMED Ould Abdel Aziz (63), aliyekuwa Rais wa Mauritania (2008–2019), amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma za rushwa alipokuwa madarakani. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Rais huyo, kwa wiki moja amekuwa mikononi mwa polisi katika mji wa Nouakchott, akikabiliwa na makosa mbalimbali aliyofanya akiwa madarakani ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi na rushwa.

“Bado hajafikishwa mahakama kushtakiwa lakini hati yake ya kusafiria ambayo ilichukuliwa wakati alipokamatwa, hajarudishiwa,” amesema mwanasheria wake Taghioullah Aida.

Rais huyo alipelekwa katika Makao Makuu ya Polisi tarehe 17 August 2020, baada ya polisi kufika nyumbani kwake na kumtaka kuondoka naye kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Rais Aziz aliachIwa na jeshi hilo saa 7:30 mchana kwa majira ya Mauritania tarehe 24 Agosti 2020 ikiwa ni siku nane baada ya kukamatwa kwake. Hata hivyo, ametakiwa kutotoka ndani ya mji aliopo sasa (Nouakchott).

Shinikizo la kukamatwa rais huyo zilichagizwa na bunge la nchi hiyo baada ya kupitia matukio mbalimbali yaliyojiri kwenye utawala wake. Tuhuma zingine anazobebeshwa rais huyo akiwa madarakani ni pamoja na matumizi mabaya ya mali za ofisi.

Taarifa zaidi zinaeleza, Rais Aziz awali aligoma kutoa ushirikiano kwa wachunguzi wa jeshi hilo na kwamba jeshi hilo lilimlazimisha kujibu maswali jambo ambalo alitekeleza.

Miongoni mwa mambo aliyokuwa hataki kuyatolea ufafanuzi zaidi ni pamoja na taasisi ya Al-Rahma iliyofunguliwa na mtoto wake.

Aziz aliingia madarakani mwaka 2008 na kuhudumia taifa hilo kwa vipindi viwili kabla ya kupokewa kijiti na rais wa sasa, Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani mwaka 2019. El Ghazouani alikuwa mtu wa karibu wa Rais Aziz na pia Waziri wa Ulinzi wakati wa utawala wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!