Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Sitaki kuwa mfalme
Habari za Siasa

Rais Magufuli: Sitaki kuwa mfalme

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amewaeleza Watanzania kwamba, hataki kuwa mfalme wa nchi hii badi mtatuzi wa kero za wananchi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Aprili 2019 wakati akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo –Kilimasera-Matemanga iliyoko mkoani Ruvuma, yenye urefu wa Kilomita 193.

Amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa kuwa, anataka kuwa mtumishi wao katika kutatua kero wanazokutana nazo.

“Nawaomba muendelee kuniombea, muniweke kwenye maombi, dua zenu, sala zenu, kila mmoja kwenye imani yake.

“Nataka niendelee kuwa mtumishi wenu na si mfalme wenu, ninataka niwe mtumishi wa kujibu kero zenu,endeleeni kuniombea,” amesema na kuongeza;

“Endeleeni pia kuwaombea viongozi wenu wakaishike zana ya utumishi wa Watanzia badala ya wao kutumikiwa, wakaelewe kwamba cheo ni dhamana, wakatambue wamepewa na Mungu wakawatumikie, wakatambue vyeo vyao wakivitumia vibaya siku moja watajibu mbele ya haki.”

Pia amewataka Watanzania kujenga utaratibu wa kushauri viongozi wa umma wanapokosea ili wajirekebishe.

 “Lakini muwashauri na kuwarekebisha walipokosea, na mkawape nguvu wale watakaokuwa wanajitahidi,” amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa kufanya mabadiliko ya kiutendaji ili kuondoa changamoto za kusua sua kwa utekelezaji wa miradi ya maji.

“Kwenye kazi za miradi ukiwa mpole haiwezi kukamilika, lazima uwe kichaa kichaa, asikie tu sauti yako, niiombe wizara yako saa nyingine lazima tuwe na mabadiliko mapana. Kakae na wataalamu wako, mainjinia wako wa maji, na katika mainjinia wamekuwa wakipafomu ovyo nchi hii ni mainjinia wa maji.  Tangia enzi za Kamwelwe nilikupeleka pale nikajua utawabadilisha,” amesema Rais Magufuli.

“ Hapa Tunduru mabarabara yote hii mpaka Namtumbo, Songea nenda mpaka Mtwara kwa kupitia Masasi ukimwambia mtu wa Ulaya au China wanatucheka sana, wanatuona hatujui kufikiria hasa kwa viongozi na watendaji wa wizara ya maji.

“Tulipokuwa tunatengeneza barabara kila sehemu tulikuwa tunajenga madaraja, yale madaraja yalikuwa yana pitisha nini? Yalikuwa yanapitisha maji, tumeshindwaje wizara ya maji kila maeneo ya mito tukachimba bwawa tukafunga mota ili yasambaze maji?”

Kuhusu barabara hiyo, Rais Magufuli amesema itasaidia kukmarisha shughuli za kichumi katika mikoa ya kusini, ikiwemo kuimarisha usafirishaji wa mazao yanayolimwa katika mikoa hiyo.

 “Barabara hii tangu tupate uhuru miaka 58 iliyoppita, kuna watu hawakuamini kama wangepita katika lami, wapo wazee wetu walifariki pasipo kuona lami. Mradi huu ni mkubwa sana hufanyika katika nchi ya Tanzania, kilomita hizi tangu tupate uhuru hazikuwa na lami lakini leo ina lami.

Rais Magufuli amesema nia yake ni kuhakikisha yale yaliyoshindikana miaka 58 iliyopita kutekelezwa katika awamu ya uongozi wake.

“Tunataka yale yalishondikana miaka 58, nataka yafanikiwe miaka 5 au miaka kumi ya awamu ya tano,” amesema Rais Magufuli.

“Fedha hizi zilizotumika tungewaambia WanaTunduru wachange wasingeweza hata kwa miaka 200, kwa sababu sisi ni wamoja, tumeikusanya fedha hii tukasema sasa ni zamu ya WanaTunduru. Lakini tulipotengeneza lami Tunduru sio kwamba Tanzania yote ina lami,  mnapopata kituo fulani sio lazima vyote mpate,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!