Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli sasa kufunga Bunge mwishoni mwa mwezi
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli sasa kufunga Bunge mwishoni mwa mwezi

Rais John Magufuli
Spread the love

BUNGE la Tanzania, sasa limeamua kufungasha vilago vyake, mwezi mmoja kabla ya muda wake wa awali uliopangwa na uongozi wa Bunge hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa iliyotolewa kwa wabunge wote wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Bunge, Steven Kigagai, imeeleza kuwa mkutano wa Bunge la 19 utafungwa rasmi tarehe 30 Mei mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba ya awali, Bunge la Jamhuri ya Muungano, lilipangwa kumaliza muda wake, tarehe 30 Juni 2020. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, siku hiyo – 30 Juni 2020 – ndipo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kufunga Bunge la Tanzania, tayari kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa 25 Oktoba 2020.

Haijaelezwa sababu za uongozi wa Bunge kuamua kumaliza mkutano wa bajeti mapema, kinyume na utamaduni wake wa miaka mingi. 

Lakini mfanyakazi mmoja wa Bunge anasema, “kupunguza huko kwa siku za mkutano wa Bunge la Bajeti, kunawezekana kuwa kunatokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Corona.

Tangu kuanza kwa mkutano huu wa Bunge, Machi mwaka huu, tayari wabunge watatu wameshapoteza maisha; jambo ambalo limesababisha baadhi ya wabunge kumtaka Spika Job Ndugai, kusitisha vikao vya Bunge hilo.

Wabunge hao waliokufa katika kipidi hiki, ni Mchungaji Gertrude Rwakatare, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM); Mwanadiplomasia wa siku nyingi ulimwenguni ambaye pia alikuwa waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Mbunge wa Sumve, Richard Mganga Ndasa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo mpya, Bajeti Kuu ya Serikali, badala ya kujadiliwa kwa wiki mzima kama ilivyokuwa huko nyuma, sasa itajadili kwa siku mbili – Alhamisi na Ijumaa. 

“Kura ya kupitisha bajeti utakaoambatana na upigaji wa kura ya wazi, utahitimishwa 22 Mei 2020” na kwamba Rais atafunga Bunge wiki moja kutoka upitishaji wa bajeti ufanyike.

Aidha, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na Rais Magufuli, wote watahutubia Bunge siku moja, wakati kwenye ratiba ya awali, Waziri Mkuu alipangwa kuhutubia Bunge tarehe 29 na rais siku inayofuata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!