Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Nitamkaba Lukuvi alipe pesa zangu
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli: Nitamkaba Lukuvi alipe pesa zangu

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, atamkaba Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ili amlipe Sh. 1 milioni fedha alizowapa wazee wawili ambao mmoja wao alidhulumiwa eneo lake. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 5 Septemba, 2018 wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, baada ya kupokea malalamiko ya kuporwa ardhi yaliyotolewa na wazee hayo.

Bibi Nyasasi Masige (mwenye kiwanja) akiwa na jirani yake wamemlalamikia Rais Magufuli kuwa, kuna tajiri aliyedhulimu kiwanja cha mmoja wao baada ya kumuuzia kiwanja cha pili kwa ajili ya kupata fedha za matibabu, na kwamba aliporudi kutoka kupata matibabu alikuta tajiri huyo amejimilikisha kiwanja cha pili.

Wazee hao walidai kuwa, mgogoro wao ulimfikia Waziri Lukuvi ambapo aliagiza bibi huyo kupatiwa kiwanja chake jambo ambalo halijafanyika hadi leo.

Kufuatia malalamiko hayo, Rais Magufuli alimtafuta Waziri Lukuvi kwa njia ya simu, na kumuagiza kumsimamisha kazi kamishna wa ardhi wa kanda hiyo kuanzia leo.

Baada ya hapo Rais Magufuli aliwakabidhi wazee hao kila mmoja Sh. 500,000 kutokana na usumbufu walioupata na kwamba, fedha hizo zitalipwa na Waziri Lukuvi. Rais Magufuli yupo mkoani Mara kwa ziara ya kikazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!