Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Kupitisha jina ‘inategemea nimeamkaje?’
Habari za Siasa

Rais Magufuli: Kupitisha jina ‘inategemea nimeamkaje?’

Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka wateule wake walio na majukumu kutokimbilia majimboni kugombea, na kwamba kupitishwa kwa majina yao kunategemea ‘siku hiyo ataamkaje.’ Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Ametoa tahadhari hiyo leo Jumatatu tarehe 22 Juni 2020, wakati akiwaapisha viongozi wapya wa Mkoa wa Arusha, aliowateua hivi karibuni.

“Ninachotaka kusema sizui kwenda kugombea lakini niwaombe mfikirie zaidi, kama una jukumu lako kubwa unafanya vizuri na watu wanakuamini, itumikie mpaka umalize. Lengo kubwa ni kuijenga Tanzania na kila mmoja anaweza kujenga kokote,” amesema Rais Magufuli.

Amewatahadharisha wateule wake, akisema kwamba, hata kama wakishinda katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaweza akabatilisha ushindi wao.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo huku akimtolea mfano IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

“Lakini nimemteua yeye awe IGP, kaondoka hapa anaenda Bunda na saa nyingine akasema nitamteua kuwa waziri, kwanza hana uhakika kama atashinda kwenye kura za maoni na inawezekana akashinda bado nikamfuta na itatokana siku hiyo nimeamkaje,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema hawazuii wateule wake kugombea, ila amewataka wajipime ubavu kama wanaweza kushinda katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM.

“Saa nyingine ni kuridhika, hamuwezi mkawa na kila kitu, lakini demokasia iko huru, kama unahakika utashinda nenda kwa spidi kubwa, nafikiri saa nyingine ni kuridhika, kila mahali unaweza kufanya maajabu kwenye nafasi yako,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the loveUSHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou...

error: Content is protected !!