Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC akihutubia wajumbe wa mkutano huo

Rais Magufuli kukabidhi uenyekiti SADC J’tatu

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli anakabidhi rasmi kijiti cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kwa Rais wa Msumbiji, Phillip Nyusi, Jumatatu tarehe 17 Agosti 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Magufuli anakabidhi uenyekiti huo wa SADC kwa Rais Nyusi, baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja wa kuongoza jumuiya hiyo, tangu alipokabidhiwa rasmi na Rais wa Namibia, Hage Geingob Agosti 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 15 Agosti 2020 na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania amesema baada ya mwaka mmoja wa mafanikio na kazi kubwa ya kuongoza jumuiya muhimu katika ukanda wa Afrika SADC, Rais Magufuli atakabidhi kijiti kwa mafanikio makubwa kwa Rais Phillip Nyusi.

Dk. Abbasi amesema, katika makabidhiano hayo, Rais Magufuli ataeleza kwa kina mafanikio ya Tanzania katika kuiongoza jumuiya hiyo.

“Rais Magufuli yeye mwenyewe ataeleza mafanikio kwa kina ya ajenda gani tuliisukuma na maamuzi gani yamefanyika kataika jumiya ya SADC na yamekuwa na manufaa gani kwa wananchi wa nchi 15 za jumuiya hiyo,” amesema Dk. Abbasi.

Makabidhiano ya Unyekiti wa SADC kwa Nchi ya Msumbiji yalianza wiki iliyopita, ambapo Alhamisi tarehe 13 Agosti 2020 , Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, alikabidhi uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC, kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, ambaye aliwakilishwa na Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Monica Clemente.

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli anakabidhi rasmi kijiti cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kwa Rais wa Msumbiji, Phillip Nyusi, Jumatatu tarehe 17 Agosti 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea). Rais Magufuli anakabidhi uenyekiti huo wa SADC kwa Rais Nyusi, baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja wa kuongoza jumuiya hiyo, tangu alipokabidhiwa rasmi na Rais wa Namibia, Hage Geingob Agosti 2019. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 15 Agosti 2020 na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania amesema baada ya mwaka mmoja wa mafanikio na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!