July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli kuhitimisha Bunge leo

John Magufuli, Rais wa Tanzania

Spread the love

SAFARI ya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoanza siku 1670 zilizopita inahitimishwa leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Bunge hilo la 11 linaloongozwa na Spika Job Ndugai lilianza safari yake rasmi tarehe 20 Novemba 2015 kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kulizindua.

Siku ya uzinduzi wa Bunge hilo, wabunge wote wa upinzani, wakiongozwa na Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni walitoka ndani ya ukumbi.

Leo Jumanne, Rais Magufuli anakwenda kulihutubia Bunge hilo ili kuruhusu kwenda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

error: Content is protected !!