Rais Magufuli awashukia watoto wa vigogo

Spread the love

RAIS John Pombe Magufuli, ameonesha kukerwa na tabia ya baadhi ya watoto wa viongozi wa ngazi za juu ‘wakubwa’ wanaojikweza kutokana na nyazifa za baba zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020 jijini Dodoma, Rais Magufuli amesema, kuna baadhi ya watoto wa marais, wanahulka ya kubeba urais wa baba zao.

Ametoa kauli hiyo wakati akimsifu Mgombea Urais wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mtoto wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Dk. Mwinyi amechaguliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kuipeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi wa Urais wa Zanzibar, jana tarehe 10 Julai 2020 na kuthibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu.

Mgombea huyo wa CCM Zanzibar, aliwashinda wanachama wengine 31, waliojitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho, kugombea Urais wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Rais Magufuli amesema Dk. Mwinyi ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, yuko tofauti na na watoto wa wakubwa, kutokana kwamba, hajaubeba urais wa baba yake.

Amesema Dk. Mwinyi ni mtu mwenye heshima, mkarimu na mpole.

“Niseme kuhusu Dk. Hussein Mwinyi, mimi namfahamu, ni tofauti sana na vijana na watoto wengi wa wakubwa, Dk. Mwinyi hajaubeba urais wa baba yake, nasema uongo,” ameuliza Rais Magufuli na kujibishwa kwa shangwe kubwa

“Ni kijana mkweli, ana heshima ana ukarimu wa hali ya juu,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, alipochaguliwa kugombea urais mwaka 2015, alimchagua Dk. Hussein Mwinyi na Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza lakini alimua kwenda na Samia.

Rais Magufuli amesema, Dk. Mwinyi hakusikitika kwa hatua hiyo, kwani alitulia na kuchapa kazi kama Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

RAIS John Pombe Magufuli, ameonesha kukerwa na tabia ya baadhi ya watoto wa viongozi wa ngazi za juu ‘wakubwa’ wanaojikweza kutokana na nyazifa za baba zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea). Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020 jijini Dodoma, Rais Magufuli amesema, kuna baadhi ya watoto wa marais, wanahulka ya kubeba urais wa baba zao. Ametoa kauli hiyo wakati akimsifu Mgombea Urais wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mtoto wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi. Dk. Mwinyi amechaguliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kuipeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!