Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli awashangaa wabunge wa upinzani wanaohamia CCM
Habari za Siasa

Rais Magufuli awashangaa wabunge wa upinzani wanaohamia CCM

Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli
Spread the love

HUKU vikao cha Chama cha Mapinduzi (CCM) vikiendelea, Mwenyekiti wa chama hicho, John Magufuli, ameoneshwa kushtuka kwa wimbi la wapinzani wanaotoka katika vyama vya upinzania na kuhamia CCM, anaandika Dany Tibason.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano wa CCM Magufuli amesema kuwa kuna kila sababu ya kuwatafakari wale ambao wanataka kuhamia CCM kwa madai kuwa uenda wakawa wametumwa kuvuruga chama hicho.

Amesema kuwa inashangaza kuona mbunge ambaye analipwa zaidi ya Sh. 12 milioni kwa mwezi anaachia mshahara wake na kujiunga na CCM jambo ambalo amesema kuwa linatia shaka

Hata hivyo amesema kuwa mpaka sasa wapo baadhi ya wabunge wa upinzani takribani 10 na madiwani saba wameomba kujiunga na CCM lakini bado wameambiwa waendelee na ubunge wao hadi watakapo kuwa wamemaliza.

Hata hivyo wajumbe wa mkutano huo waliokuwa wakizungumza na mwenyekii wao walipaza sauti wakimtaka mwenyekiti kuakubalia wabunge hao waotoka upinzani wajiunge na CCM kwa madai kuwa watakuwa wamepunguza nguvu za upinzani.

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa kinachofanywa na CCM kwa sasa ni kutaka kudhoofisha nguvu ya upinzani jambo ambalo ni hatari katika masuala mazima ya demokrasia.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online kwa mashariti ya kutokutajwa majina walitaka ofisi ya spika ieleze wabunge ambao wamekuwa wakiachia ngazi na kwa wale ambao wamekuwa na mikopo hiyo mikopo inalipwaje na mpaka sasa ni wabunge wangapi wamerejesha mikopo na asiporejesha zitachukuliwa hatua gani.

Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM taifa amekiri kutumia sera za wapinzani katika kutekeleza matakwa ya wananchi huku akiwataka wanachama wao kwa sasa wana mikakati gani kwani kwa sasa kinachotekelezwa ni ilani ya wapinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!