Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli awakabidhi Tausi marais wastaafu, JK amkumbuka Msukuma
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli awakabidhi Tausi marais wastaafu, JK amkumbuka Msukuma

Rais John Magufuli akimkabidhi Mama Nyerere tausi wake
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli, amewakabidhi marais wastaafu wa nchi hiyo ndege aina ya Tausi 25 kwa kila mmoja, ikiwa ni ishara ya kuenzi na kutambua utumishi wao katika Taifa hilo lililoanza kujitawala tarehe 9 Desemba 1961. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumamosi tarehe 30 Mei, 2020 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwamo marais hao wastaafu wakiwa na wake na familia zao.

Marais hao ni; Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete huku Mama Maria akipokea Tausi hao kwa niaba ya mume wake, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pia, Rais Magufuli amesaini hati maalum za makabidhiano hayo ya Tausi ambao kila mmoja atakwenda kuwafuga maeneo watakayopanga wao huku akiwapa na kilo 100 kila mmoja za chakula.

Mara baada ya kumaliza kuwakabidhi, Rais Magufuli akapata wasaa wa kuzungumza machache ambapo ameanza kwa kuwashukuru wastaafu hao kwa kwa kukubal kwenda kuchukua Tausi hao.

“Tausi hawa wana historia ndefu, Tanzania haikuwahi kuwa na Tausi bali waliletwa na Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) enzi za utawala wake na wametunzwa vizuri na marais wastaafu,” amesema Rais Magufuli

Amesema, baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka, alimkabidhi Mzee Mwinyi ambaye naye baada ya kumaliza muda wake wa miaka 10 mwaka 1995 akawakabidhi kwa Mzee Mkapa  na mwaka 2005 hadi 2015 waliwatunzwa na Mzee Kikwete.

 

Rais Magufuli amesema, alipokwenda Ikulu, Kikwete alimweleza kwamba hao ndege wanataga mayai mengi lakini huwa hawayalalii vizuri na alimweleza, “Kuna mfanyakazi hapa tena msukuma mwenzako, atafute ‘incubator.”

Amesema, alipoingia Ikulu, “nikamwelewa Mzee Kikwete, nilipoingia, yule msukuma nikamfukuza kwanza, baadaye tukaleta wataalamu wa wanyama mwanajeshi, kuna siku nikaambiwa na wataalamu kuna mayai zaidi ya 1000.”

Rais Magufuli amesema, baada ya kupatikana Tausi hao, “kweli ilinigusa na wazee hawa waliwapenda hawa wanyama na baba wa taifa aliwapenda.”

Amesema, kutokana na hilo, ameamua kuwatoa ndege 25 kwa kila Rais mstaafu ambapo watasafirishwa kuanzia leo na endapo ikitokea wakafa wakiwa njiani basi watabadilishwa.

“Hizi ni nyama za serikali na ndiyo maana nimesaini hati za makabidhiano kabisa ambazo mmeruhusiwa kuwachukua na watu wakija kutembelea makazi yenu watafurahia kuwaona urithi ulioletwa na baba wa taifa mnawatunza,” amesema.

Kikwete akizungumza kwa niaba ya wanzake, ameanza kwa kushukuru, “dhati kwa kutupatia hawa ndege, tulikuwa tunawatamani, lakini ukitoka nao ukafika Msoga (kijijini kwake-Bagamoto-Pwani) watasema umepora.”

Pia alipomzungumzia mfanyakazi aliyefukubwa, amesema, “mimi sikukwambia umfukuze yule Msukuma ambaye hakununua ‘incubator,’ ila nilieleza masikitiko yangu,” kwa maelekezo ambayo nilikuwa nayatoa lakini hawayatekelezi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!