Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari Rais Magufuli awaapisha warithi wa Makonda, Mnyeti
HabariHabari MchanganyikoTangulizi

Rais Magufuli awaapisha warithi wa Makonda, Mnyeti

Joseph Mkirikiti, akiapa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua wakiwemo wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam na Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Viongozi hao wameapishwa leo Alhamisi tarehe 16 Julai 2020 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma baada ya kuwateua jana Jumatano.

Walioapishwa ni; Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Paul Christian Makonda.

Soma zaidi hapa

Makonda kujitosa ubunge, mjadala waibuka

Pili, Rais Magufuli amemwapisha Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kuchukua nafasi ya Alexander Pastory Mnyeti.

Tatu, Rais Magufuli amemmwapisha Paulo Mshimo Makanza kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Awali, Makanza alikuwa Afisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na anachukua nafasi ya Kunenge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Soma zaidi hapa

JPM atengua Ma-DC, RAS, DED na RC akiwemo Makonda

Pia, Rais Magufuli amemwapisha Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General).

Gabriel Pascal Malata, Wakili Mkuu wa Serikali

Kabla ya kuteuliwa na Rais tarehe 10 Julai 2020, Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dk. Julius Clement Mashamba.

Rais Magufuli amemwapisha Dk. Boniface Luhende kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya kiapo hicho, Dk. Luhende alikuwa Mhadhiri katika Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Malata ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Aboubakar Kunenge, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli amemwapisha Dk. Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Dkt. Maduhu Isaac Kazi, Mkurugenzi Mtendaji (TIC)

Awali, Dk. Kazi alikuwa meneja wa idara ya sera za kibajeti na madeni wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Dk. Kazi amechukua nafasi ya Godffrey Idelphonce Mwambe.

Pia, Rais ameshuhudia uapisho wa wakuu wa wilaya za Kongwa, Kiteto, Chunya, Moshi na Hanang uliofanywa na Wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Manyara na Dodoma.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!