Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli awa kivutio Sauzi, ampiga picha Kikwete, Ramaphosa
Habari za Siasa

Rais Magufuli awa kivutio Sauzi, ampiga picha Kikwete, Ramaphosa

Spread the love

RAIS John Magufuli leo Jumamosi Mei 25, 2019, amekuwa kivutio nchini Afrika Kusini baada ya kugeuki fani ya kupiga picha katika hafla ya kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo leo, Cyril Ramaphosa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa nchini mbalimbali, akiwemo Rais Magufuli na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kiwete kuliibuka matukio mengi ya kufurahisha.

Moja kati ya matukio hayo ni kitendo cha Rais Magufuli kutumia simu ya mkononi kuwapiga picha Rais Ramaphosa na Kikwete.

Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi katika mitandao ya kijamii na kushangazwa na Rais Magufuli jinsi alivyoshikilia vyema simu hiyo na kuwapiga picha wawili hao.

Viongozi hao walionekana kufurahia tukio hilo wakiwemo baadhi ya marais wa mataifa mengine waliokuwa pembeni yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!