Rais Magufuli atua Dar, achangisha harambee Ubungo

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea Makao Makuu Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 imesema akiwa Ubungo, Rais Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.

Amesema, Rais Magufuli amefurahishwa kwake na kazi nzuri inayoendelea, pia amewasalimu wananchi wakiwemo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kando ya eneo la mradi huo.

Rais John Magufuli

Akizungumza kwa niaba viongozi wa vyama vya siasa na vijana wa Ubungo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Ubungo, Edwin Cyprian Mbena amempongeza, Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kutekeleza vizuri na kwa vitendo Ilani ya CCM ikiwemo ujenzi wa barabara za juu katika eneo hilo, na ameeleza kuwa mradi huo umeleta heshima na unawanufaisha wananchi wa Ubungo na Jiji zima la Dar es Salaam.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaamini vijana na kuwapa nafasi za uongozi na amemuahidi kuwa vijana wamekubaliana kutomuangusha kwa kuhakikisha wanachapakazi na kusimamia maslahi mapana ya Taifa bila kubagua.

Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Ubungo kwa kupata mradi huo na ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inatumia zaidi ya Sh. 240 bilioni kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo na pia inajenga barabara ya njia nane (Kimara – Kibaha) kwa kuwa imedhamiria kuibadilisha Tanzania. Amewataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi hizo.

Baada ya kuwasalimu wananchi hao, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia ununuzi wa pikipiki ya miguu mitatu kwa ajili, Nyangoma James ambaye ni mwenye ulemavu, na amefanikiwa kukusanya Sh.8,750,000 zikiwemo Sh.5 milioni  alizotoa yeye mwenyewe.

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea Makao Makuu Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 imesema akiwa Ubungo, Rais Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma. Amesema, Rais Magufuli amefurahishwa kwake na kazi nzuri inayoendelea, pia amewasalimu wananchi wakiwemo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kando ya eneo la mradi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Hamisi Mguta

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!