Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Magufuli atia ‘tumbo joto’ taasisi za serikali
Habari Mchanganyiko

Rais Magufuli atia ‘tumbo joto’ taasisi za serikali

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli ameagiza mashirika na taasisi za umma, zitakazoshindwa kupeleka gawio serikalini hadi kufikia Julai mwaka huu, zichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ametoa agizo hilo leo tarehe 21 Mei 2019 wakati akikabidhiwa hundi ya kiasi cha Sh. 2.1 bilioni, kama gawio kutoka Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL).

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, amemuagiza Msajili wa Hazina, Athuman Mbuttuka kuwaandikia barua viongozi wa taasisi zinazotakiwa kutoa gawio serikalini, huku akimtaka kutowafumbia macho watakaokiuka agizo hilo.

“Lazima msajili wa hazina uwe mkali sana kwenye hili, ili mashirika yote 253 kabla ya mwezi wa saba haujaisha yote yawe yametoa gawio, kama mpaka jeshi yanatoa gawio mil 700 kupitia Suma JKT, , nataka taasisi zinazotakiwa kutoa gawio kwa mujibu wa sheria, waandikiwe barua na nakala ipelekwe serikalini . Watimize wajibu wao,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya Mbuttuka kutajwa idadi ya mashirika ya umma yaliyopeleka gawio lao serikalini, ambapo alisema takribani mashirika 8 kati ya 253 ndiyo yaliyotekeleza agizo hilo.

“Lazima tufuate sheria ili yatoe au yaondoke, hatuwezi kwenda kwa mtindo huu . Wao kila siku wanakuja kushuhudia TTCL inatoa gawio wao hawatoi, kila mwaka wanasema wanapata hasara lakini hawafungi biashara,” amesema Rais Magufuli.

Awali, Mbuttuka alitaja mashirika yaliyotoa gawio serikalini, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililotoa milioni 600, Suma JKT (700 milioni) na TTCL lililotoa gawio la 2.1 bilioni.

“Makampuni walisolipa gawio watekeleze mikataba tuliyosaini, kwa kipindi hiki hadi Juni tunatgemea mashirika kuchangia, niwakumbushe wasiochangia kutimiza wajibu wao.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza TTCL kumuorodheshea majina ya watumishi wa serikali wanaotumia mtandao wa TTCL, huku akiwataka wasiotumia mtandao huo kuanza kutumia mara moja.

Rais Magufuli amesema “Sio ofisi ya waziri mkuu, makamu wa rais, wizara ya fedha hata wizara yako mawasiliano na uchukuzi haikutajwa hapa is ni aibu, tunazungumza maneno kuliko vitendo, sijui nifanyaje, mimi simu yangu niliyonayo hapa ni TTCL najilipia mwenyewe ni lazima tuwe wazalendo tusipokuwa tutachezewa mno.

“Niorodheshee wenye namba za TTCL ili baada ya mwezi mmoja tutaangalia viongozi wa serikali wanaolipwa mshahara wa serikali hana namba ya TTCL. Na zile zinazotumika isiwe anatuma sms halafu line wanafunga, ombi kubwa ni lazima tujali vitu vyetu,” amesisitiza Rais Magufuli.

Pia, ameagiza Wizara ya fedha kuiongezea mtaji TTCL haraka iwezekanavyo ili shirika hilo lizidi kufanya kazi kwa ufanisi na kujiongezea mapato.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!