Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ateua Mwenyekiti NBS
Habari za Siasa

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti NBS

Rais John Magufuli
Spread the love
RAIS John Magufuli amemteua Dk. Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 25 Septemba 2019 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu.

Taarifa ya Msigwa inaeleza kuwa Dk. Msengwa ambaye ni Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anachukua nafasi ya Andrew Massawe, baada ya kumaliza muda wake.

“Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 19 Septemba 2019,” inaeleza taarifa ya Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!