Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ataja kilichomng’oa Gambo
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli ataja kilichomng’oa Gambo

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, amemfukuza kazi Mrisho Gambo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wenzake wawili, kutokana na kutotekeleza maagizo yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe 19 Juni 2020, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Gambo, Gabriel Daqarro ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Dk. Maulid Madeni, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Rais Magufuli ametaja sababu hizo leo Jumatatu tarehe 22 Juni 2020, wakati akiwaapisha viongozi wapya aliowateua kwa ajili ya kujaza nafasi zao.

Rais Magufuli amesema, ametengua uteuzi wa viongozi hao kutokana na kutofurahishwa na mienendo yao, ikiwemo kugombana kwa takribani miaka miwili.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Mrisho Gambo

“Mimi saa nyingine nasikitikaga sana unapoona watu uliowateua na ukawaapisha na kuwaamini kwa niaba ya Watanzania, wanapoenda kule hawafanyi kadri ya viapo, mtakumbuka hivi karibuni nilitengua uteuzi wa wote kuanzia, sababu katika kipindi cha miaka mwili walikuwa wanagombana tu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Kila mmoja ni bosi anatengeneza mizengwe kwa mwenzake sikufurahishwa, walifanya kazi zao lakini waliniudhi wao kutoshirikiana na kufanya yale ambayo nimewaagiza, sasa nimewateuwa ninyi sitaki yakajitokeze hayo.”

Rais Magufuli amewaagiza viongozi wapya aliowaapisha kujaza nafasi zao, kwenda kufanya kazi kwa mujibu wa viapo vyao, ili changamoto zilizojitokeza zisijirudie tena.

Viongozi aliowaapisha ni, Iddi Kimanta, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kena Kihongosi, Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Dk. John Pima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!