March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli asifu baraza lake

Rais John Magufuli

Spread the love

SIKU saba baada ya mawaziri na manaibu waziri kuapishwa kutumikia nafasi hizo, Rais John Magufuli amewasifu kwamba wameanza kazi vizuri. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Desemba 2020, wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri cha muhula wake wa pili wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, kisha ufunguzi wake kurushwa mubarasha kupitia Shirika la Habari Tanzania (TBC).

“Waheshimiwa wajumbe karibuni, makamu wa rais, waziri mkuu na wajumbe wote, basi tuanze kikao chetu, hii leo tumekutana hapa wote nitatoa mwelekeo lakini kwa ujumla mmeanza vizuri sana,” amesema Rais Magufuli.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa. Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi. Mawaziri 23 pamoja na manaibu wao.

Mawaziri 21 pamoja na manaibu waziri 23 waliohudhuriwa katika kikao hicho, waliteuliwa tarehe 5 Desemba 2020 na kuapishwa na Rais Magufuli katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma tarehe 9 Desemba mwaka huu.

Kikao hicho kilianza saa 10: 24 asubuhi kwa Rais Magufuli kumuapisha Rais wa Zanzibar, Dk.  Mwinyi kuwa mjumbe wa baraza hilo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Mawaziri waliohudhuria leo ni, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Maryprisca Mahundi (naibu). Waziri  wa Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, George Mkuchika  na Ndejembi John (naibu).

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Angelina Mabula (naibu). Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa na Abdallah Ulega (naibu).

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Ummy Nderiananga na Patrobas Katambi (manaibu). Waziri wa Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mwigulu Nchemba na Gefrey Pinda (naibu). Waziri wa  Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki na Pauline Gekul (naibu).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro na Mary Massanja (naibu). Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jaffo na Dk. Festo Lugange na David Silinde (manaibu).

Waziri wa  Nishati, Dk. Medard Kalemani  na Stephen Byabato (naibu). Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda  na Hussein Bashe (naibu). Waziri wa Madini, Doto Biteko na Prof. Shukrani Manya (naibu).

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene na Hamis Hamza Hamis (naibu). Waziri wa Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu  na Mwita Waitara (naibu).

Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia na Habari, DK. Faustine Ndugulile  na Kundo Mathew (naibu).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima na Dk. Godwin Mollel (naibu). Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamriho na Msongwe Kasekenya (naibu).

Waziri wa Viwanda na Biashara, Geofrey Mwambe na Kigahe Silaoneka (naibu). Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Kipanga Omary (naibu).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na William Ole Nasha (naibu) na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango na Mwanaidi Ali Hamis (naibu).

error: Content is protected !!