Katika safari hiyo Rais Magufuli alitumia kuzungumza na abiria waliopanda ndege hiyo ikiwa pamoja na kupiga nao picha mbalimbali kama kumbukumbu.
Ndege hiyo ilizua gumzo mitandaoni wiki iliyopita baada ya kusimamisha huduma kwa matengenezo ya kawaida kabla ya kuanza tena safari zake za kawaida za Dar es Salaam, Moshi na Mwanza.
Kitendo cha Rais Magufuli kutumia ndege hiyo kubwa zaidi nchini, ni kuwahakikishia wananchi kuwa ipo salama na wamezungumza na kuwapongeza wananchi waliosafiri nao pamoja.
Rais Magufuli baada ya kushuka uwanja wa Ndege wa Mwanza alikwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akapopokewa na viongozi kadhaa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Wakati akitoka katika hospitali hiyo alisimamisha msafara wake na kuzungumza na wanafunzi wa Shule Msingi Mongella iliyopo eneo la Bugando waliokuwa wamesimama pembeni mwa barabara.
“Mmekuja kufanya nini hapa,” Rais Magufuli aliwauliza swali wanafunzi hao. Kwa sauti ya pamoja, wanafunzi hao wakajibu “Tumekuja kukuona”
Baada ya jibu hilo, Rais Magufuli aliwashukuru wanafunzi hao na kuwaambia, “Nitarudi siku nyingine kuonana na kuzungumza nanyi. Leo nimefika hapa kumuona mgonjwa wangu ambaye amelazwa hapa hospitalini. Endeleeni kuwaombea wagonjwa waliolazwa hospitalini.”
Leave a comment