Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli akagua magari 130 yaliyotaifishwa, atoa maagizo
Habari za Siasa

Rais Magufuli akagua magari 130 yaliyotaifishwa, atoa maagizo

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekagua magari yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi kisha kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani Jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema, Rais Magufuli amefanya ukaguzi huo leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020.

Idadi ya magari hayo ni 130 yakiwemo makubwa na madogo yalikamatwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kisha wahusika kufikishwa mahakamani na Mahakama kutoa uamuzi wa kuyataifa.

Akizungumza baada ya kuyakagua, Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na wote waliohusika kuwakamata waliokuwa wanajihusisha na vitendo hivyo (ikiwemo biashara haramu ya meno ya tembo) na ameagiza magari hayo yagawanywe katika taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali.

Rais Magufuli amewapongeza wananchi waliojitokeza kutoa taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watu waliokuwa wanafanya uhalifu kwa kutumia magari hayo na amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!