Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli aifariji familia ya Mkapa
Habari za Siasa

Rais Magufuli aifariji familia ya Mkapa

Rais John Magufuli akimpa pole Mama Anna Mkapa. Pembeni Mama Janeth Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwa Hayati Rais wa awamu ya tatu wa nchi hiyo, Benjamini William Mkapa, Masaki jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Magufuli akiwa ameambatana na mkewe, Janeth wametoa mkono wa pole kwa Anna, mjane wa Mkapa, ndugu, jamaa na marafiki waliopo msibani hapo.

Mara baada ya kuwasilia, Rais Magufuli na Janeth walikwenda moja kwa moja eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo.

Wawilia hao baada ya kuamliza, walikwenda ndani kuwasafiri wafiwa akiwemo Anna.

Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Mkapa utaagwa kwa siku tatu katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuanzia kesho Jumapili hadi Jumanne tarehe 28 Julai 2020 kisha utasafirishwa kwenda kijijini kwake, Lupaso Mkoa wa Mtwara kwa maziko yatakayofanyika Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!