Rais CAF aguswa na ajali ya MV Nyerere – MwanaHALISI Online
The newly elected Confederation of African Football President Ahmad Ahmad addresses a news conference after his victory at the African Union headquarters in Ethiopia's capital Addis Ababa

Rais CAF aguswa na ajali ya MV Nyerere

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi msiba wa waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi kati ya Ukara na Bugorara, Ukerewe. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Rais wa CAF, Ndugu Ahmad ametoa pole kwa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli na watanzania kiujumla na pia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo mzito uliosababisha majonzi makubwa kwa Watanzania.

“Naungana na Watanzania na Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa msiba huo mzito kwa Tanzania,” alisema Rais wa CAF.

Wakati huohuo, Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa waliofariki katika ajali hiyo.

Karia amesema ni huzuni kubwa kwa Taifa na Watanzania kwa ajali hiyo iliyopoteza wapendwa wetu.

Amesema ajali hiyo imepoteza wana familia ya Mpira wa miguu ambao walikuwa wakifuafilia ama mashabiki wa mchezo huo lakini pia ajali hiyo imepoteza nguvu kazi ya Taifa.

TFF inaungana na Ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupoteza wapendwa wao. Pia inawapa pole na kuwatakia afya njema majeruhi waliookolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana.

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi msiba wa waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi kati ya Ukara na Bugorara, Ukerewe. Anaripoti Kelvin Mwaipungu ... (endelea). Rais wa CAF, Ndugu Ahmad ametoa pole kwa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli na watanzania kiujumla na pia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo mzito uliosababisha majonzi makubwa kwa Watanzania. “Naungana na Watanzania na Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa msiba huo mzito kwa Tanzania,” alisema Rais wa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Kelvin Mwaipungu

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube