Friday , 29 March 2024
Kimataifa

Rais Brazil atupwa jela

RAIS wa zamani wa Brazil, Lula da Silva alipotembelea Tanzania wakati wa madaraka yake
Spread the love

RAIS wa zamani wa Brazil, Lula da Silva, amehukimiwa kifungo cha miaka tisa na nusu gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa, anaandika Catherine Kayombo.

Silva anakuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo kufugwa gerezani. Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza 14 Septemba 2016.

Alidaiwa kuwa alijihusisha na rushwa katika kampuni ya umma ya mafuta ya Petrobras.

Kiongozi huyo wa aliyeiongoza Brazil kati ya mwaka 2003 na 2010 amepatikana pia na hatia ya kupokea mlungula wa zaidi ya dola za Marekani 100 milioni kwa ajili ya malipo ya ukarabati wa ghorofa ya mapumziko kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil iitwayo OAS.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, rushwa aliyojihusisha nayo rais Silva, ndio kubwa katika historia ya nchi hiyo.

Jaji wa mahakama kuu ya Brazil, Sergio Moro, amesema kuwa amejiridhisha na ushahidi muhimu uliotolewa na mashuhuda wawili waliothibitishia mahakama yake kuwa Silva alipokea mamilioni hayo ya dola.

Silva alihukumiwa kwenda gerezani Jumatano ya tarehe 12 Julai 2017.

Kufuatia hukumu hiyo, Silva amesema hastahili adhabu hiyo kwa kuwa hajafanya kosa linalo sababisha kustahili hukumu hiyo. Mawakili wake wanajiandaa kukata rufaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!