Raia wa Vietnam atupwa jela miaka 20

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh. 100 milioni Bui Hoa, Raia wa Vietnam baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kukutwa na kucha na meno ya Simba, anaandika Faki Sosi.

Hukumu hiyo imetolewa na Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu baada ya mshitakiwa huyo kukiri kukutwa na nyara hizo za serikali kinyume cha sheria.

Awali, Helleni Moshi, Wakili wa Serikali Mwandamizi alisema mshitakiwa huyo alikutwa na nyara hizo tarehe 8 Januari mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jinini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa siku hiyo, Hoa alikutwa na kucha tano za simba na meno manne yote yakiwa na thamani ya Dola za Marekani 4900 (takribani Sh. 10,647,700 za Tanzania), mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh. 100 milioni Bui Hoa, Raia wa Vietnam baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kukutwa na kucha na meno ya Simba, anaandika Faki Sosi. Hukumu hiyo imetolewa na Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu baada ya mshitakiwa huyo kukiri kukutwa na nyara hizo za serikali kinyume cha sheria. Awali, Helleni Moshi, Wakili wa Serikali Mwandamizi alisema mshitakiwa huyo alikutwa na nyara hizo tarehe 8 Januari mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jinini Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa siku…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube