Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Raia wa Tanzania, DRC wapigwa marufuku kuingia Uingereza
Habari MchanganyikoTangulizi

Raia wa Tanzania, DRC wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Spread the love

UINGEREZA imepiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kuingia nchini humo, ili kuzuia maambukizo ya aina mpya ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu …. (endelea).

Katazo hilo linaanza kwa wasafiri wote waliotoka ama kupita nchini Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ndani ya siku 10 zilizopita.

Waziri wa uchukuzi wa Uingereza, Grant Shapps, jana Alhamisi tarehe 21 Januari 2021, ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, “ili kusaidia kuzuia kuenea kwa aina ya COVID-19 iliyogundulika Afrika Kusini, tunapiga marufuku abiria wote wanaoingia kutoka Tanzania na DRC kuanzia saa 10 alfajiri kesho (Ijumaa).”

Hata hivyo, Shapps amesema, raia wa Uingereza na Ireland na wale kutoka mataifa mengine ambao wenye wanabali vya ukaazi, wataruhusiwa kuingia nchini humo, ila kwa sharti la kujitenga nyumbani pamoja na familia zao kwa muda wa siku 10 baada ya kuwasili.

(To help to stop the spread of the COVID-19 variant identified in South Africa, we are banning all arrivals from Tanzania and Democratic Republic of Congo from 4am tomorrow.

Tanzana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigiwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini humo kama hatua za kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini Afrika kusini.

Awali, mwezi huu mataifa mengine 11 ya Afrika yalipigwa marufuku kama hiyo. Mataifa hayo, ni Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini, Zambia, Malawi, Lesotho, Msumbiji na Angola, Shelisheli na Mauritius.

Abiria kutoka Afrika Kusini, walipigwa marufuku kuingia Uingereza, tarehe 24 Desemba mwaka jana.

Taifa la Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yanakabiliana na janga la virusi vya corona kwa kiwango kikubwa na uchumi wake ukiwa umeyumba kutokana na wimbi la kwanza la virusi mambukizi.

Wakati Uingereza ikitangaza kupiga marufuku raia wa Tanzania na DRC kuingia nchini humo, Ujerumani na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya, walikuwa wakijadiliana uwezekano wa kufunga mipaka yao.

Serikali ya Tanzania imeondoa sharti wageni wanaoingia nchini humo kukaa karantini kwa muda wa siku 14, hata hivyo wanaowasili wote wanapimwa joto na endapo wataonesha dalili za COVID-19 ndio watahitajika kujitenga kwa muda wa siku 14.

Akitoa ujumbe wa shukurani kwa viongozi wa dini, Rais John Magufuli, aliwataka Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu ili aliepushe taifa na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!