Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Raia wa Nigeria, Lativia wadakwa na dawa za kulevya
Habari Mchanganyiko

Raia wa Nigeria, Lativia wadakwa na dawa za kulevya

Spread the love

JESHI la Polisi, Kitengo cha Kuzuia Kupambana na Dawa za Kulevya, limewatia mbaroni raia wawili wa Nigeria na Raia wawili wa Walativia wakiwa na kilogram 20 za dawa za kulevya aina ya Heroin. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na Vyombo vya Habari leo tarehe 23 Aprili 2019, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP), Alhaji Salim Kabaleke amesema, watuhumiwa hao wamekamatwa nchini wakiwa kwenye mikakati ya kusafirisha dawa hizo.

Watuhimiwa hao ni Linda Mazule, Raia wa Lativia aliyekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Julias Nyerere tarehe 17 Aprili mwaka 2019.

Wengine ni Martin Plavin, Raia wa Lativia ambaye aliingia nchini pamoja na Mazule.

Pia, Henry Ugwuanyi na Onyebuchi Ogbu Wanaijeria, wote walikamatwa kwenye msako wa kikosi hicho.

Kamanda Kabaleke amesema kuwa, watuhumiwa hao walifika nchini wakijihusisha na biashara ya dawa kulevya, walikuwa wakiishi maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Amewasihi wananchi kujijengea tabia ya kutoa taarifa wakiona wageni wapo nchini bila kuwa na shughuli maalum.

Amemtaja Ogbu, aliyekuwa akijifanya ni mchungaji lakini hana kanisa wala hana shughuli nyengine zaidi ya biashara za dawa ya kulevya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!