SHULE ya Msingi Emaco Vision English Medium ya mjini Geita mkoa wa Mwanza imepata pigo baada ya kuondokewa na wanafunzi wake sita waliofariki duniani kwa kupigwa na radi wakati wengine 25 wakijeruhiwa kwenye tukio hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Tukio hilo la kusikitisha limetokea asubuhi ya leo tarehe 17 Oktoba 2018, ambapo wanafunzi hao wa darasa la pili na la tatu walipatwa na mkasa huo wakiwa darasani.
Taarifa za tukio hilo zimethibitishwa na Ofisa Elimu Msingi wilaya ya Geita, Yese Kanyuma akieleza kuwa, radi hiyo imetokea kutokana na mvua kubwa iliyonyesha asubuhi ya leo.
Kanyuma ameeleza kuwa, majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu.
Leave a comment