Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Profesa Ndalichako aitaka HESLB kujiandaa kutoa mikopo 
Elimu

Profesa Ndalichako aitaka HESLB kujiandaa kutoa mikopo 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru akifafanua jambo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati alipofanya ziara kwenye ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam
Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kujiandaa kuwalipa wanafunzi mikopo wakati wowote vyuo vitakapofunguliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Profesa Ndalichako, ametoa maagizo hayo leo Jumatatu, tarehe 18 Mei, 2020 mara baada ya kukagua ofisi mpya za bodi hiyo na kuzungumza na menejimenti ya bodi hiyo zilizopo eneo la Tazara jijini  Dar es Salaam.

”Katika kipindi hiki ambapo vyuo vya elimu ya juu vimefungwa, HESLB ihakikishe inatumia muda huu kufanyia kazi changamoto zote za wanafunzi ili vyuo vitakapofunguliwa malipo ya mikopo ya wanafunzi yafanyike kwa wakati,” amesema Profesa Ndalichako.

Waziri huyo ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais wa Tanzania, John Magufuli kusema endapo takwimu za ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) itaendelea kushuka, anakusudia kuvufungua vyuo vyote ili wanafunzi warejee vyuoni kuendelea na masomo.

Vyuo vikuu na vya kati, vilifungwa tangu tarehe 18 Machi, 2020 kutokana na ugonjwa wa corona.

Katika mazungumzo yake na manejimenti ya HESLB, Profesa Ndalichako ameipongeza bodi hiyo kwa kutekeleza agizo la Serikali la kuhakikisha taasisi zote za umma zinahamia kwenye majengo ya Serikali ili kupunguza gharama.

“Ninaamini hapa mtafanya kazi kwa utulivu na kutaongeza ufanisi katika kazi,” amesema Profesa Ndalichako.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu wakimsikiliza Waziri qa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) alipofanya ziara kwenye Bodi hiyo

 

Profesa Ndalichako pia alitumia kikao hicho kuwakumbusha watumishi wa HESLB kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema bodi hiyo ipo tayari kuwahudumia wanafunzi muda wowote vyuo vitakapofunguliwa kwa kuwa fedha zinazohitajika, mifumo na taarifa za wanafunzi zipo.

Badru amesema, taasisi yake inakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kwa kushirikisha wadau wakiwemo wanafunzi kupitia shirikisho lao, TAHLISO.

Kuhusu urejeshaji wa mikopo iliyoiva, Badru amesema Sh. 160 bilioni zimekusanywa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, Julai 2019 hadi Aprili 2020.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watanzania wasio na uwezo na pia kukusanya mikopo iliyoiva iliyotolewa na Serikali tangu mwaka 1994/95.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!