Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Profesa Mukandala aburuzwa kortini 
Habari Mchanganyiko

Profesa Mukandala aburuzwa kortini 

Prof. Rwekaza Mukandala, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Spread the love

ALIYEKUWA mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa, Alphonce Lusako, amemburuza mahakamani, Makamu Mkuu wa  chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala akimtuhumu kumkatisha masomo bila kufuata utaratibu, anaandika Hellen Sisya.

Mukandala anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kumfukuza chuo Lusako ambaye inadaiwa alifukuzwa chuoni hapo pasipo kufuata taratibu za kisheria.

Katika kesi hiyo ya madai namba 71 ya mwaka 2017 ambayo imetajwa leo hii mbele ya Hakimu  Oswad wa mahakama ya wilaya Kinondoni jijini Dar es salaam .

Lusako anaiomba mahakama itoe adhabu kwa Profesa Mukandala pamoja na chuo hicho ya kumlipa Sh. millioni 600 kama fidia kwa kuwa wamemshushia heshima katika jamii pamoja na kumkosesha nafasi ya kupata elimu tangu mwaka 2012.

Mbali na kiasi hicho cha pesa, Lusako pia anawadai fidia ya Sh millioni tano, kwa ajili ya gharama zote ambazo alizotumia kwa ajili ya ada pamoja na pesa ya matumizi  binafsi akiwa chuoni hapo tangu mwaka jana mwishoni mpaka mapema mwaka huu alipofukuzwa.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena  Septemba 7  mwaka huu ambapo  Lusako anawakilishwa na wakili msomi Seka John na kwa upande wa Profesa  Mukandala pamoja na chuo wanawakilishwa na wakili msomi Zabibu Abdalaah.

Lusako alifukuzwa chuoni hapo kwa mara ya kwanza  mwaka 2012 akituhumiwa kufanya kosa la kinidhamu ambapo baada ya kukaa nyumbani kwa takribani miaka mitano, hatimaye October mwaka jana alifanikiwa tena kupata nafasi ya kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu chuoni.

Alikuwa akisoma shahada ya sheria, lakini mapema mwaka huu chuo hicho kilimfukuza tena kwa mara ya pili kwa madai kuwa alikuwa amedahiliwa chuoni hapo kimakosa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!