Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CUF Zanzibar, Faki Suleiman Khatib

Profesa Lipumba amsimamisha kigogo CUF

Spread the love

PROFESA Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti  wa Chama Cha Wananchi (CUF), kwa kutumia mamlaka ya kikatiba,  amemsimamisha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa chama hicho, Faki Suleiman Khatib. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo wa Profesa Lipumba, ameuchukua zikiwa zimepita siku tango tangu Baraza Kuu la CUF lilipomsimamisha Makamu Mwenyekii wake upande wa Zanzibar, Abbas Juma Muhuzi.

Muhuzi alisimamishwa tarehe 28 Juni 2020 baada ya kukutwa na makosa ya ukiukwaji wa maadili ya uongozi.

        Soma zaidi:-

Leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020, taarifa iliyotolea na Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma, Mohamed Ngulangwa imesema, uamuzi aliouchukua Profesa Lipumba ni kutekeleza agizo la Baraza Kuu la kuondoa mapungufu na kuimarisha kamati tendaji.

“Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar itajazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linalotarajiwa kuketi mwishoni mwa mwezi huu,” amesema Ngulangwa.

Prof. Ibrahim Lipumba

Amesema, Profesa Lipumba amemteua, Nadhira Ali Haji kuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Haroub Mohammed Shamis ambaye alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Ngulangwa amesema, mwenyekiti ameyafanya hayo asubuhi ya leo Jumamosi Zanzibar kwenye ziara fupi ya kumtambulisha Shamis na kushughulikia maagizo aliyopewa na Baraza Kuu lililoketi wiki iliyopita  jijini Dar es Salaam.

PROFESA Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti  wa Chama Cha Wananchi (CUF), kwa kutumia mamlaka ya kikatiba,  amemsimamisha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa chama hicho, Faki Suleiman Khatib. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Uamuzi huo wa Profesa Lipumba, ameuchukua zikiwa zimepita siku tango tangu Baraza Kuu la CUF lilipomsimamisha Makamu Mwenyekii wake upande wa Zanzibar, Abbas Juma Muhuzi. Muhuzi alisimamishwa tarehe 28 Juni 2020 baada ya kukutwa na makosa ya ukiukwaji wa maadili ya uongozi.         Soma zaidi:- Kigogo CUF yamkuta, asimamishwa Leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020, taarifa iliyotolea na Mkurugenzi wa Habari Uenezi na…

Review Overview

User Rating: 2.5 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!